PremierBet Tanzania Usain Bonus Ad

Habari za Mastaa

Blach Chyna awatolea nje Kardashians

on

 Blac Chyna afunguka kwenye mahojiano aliyofanya na Daily Mail Tv na kusema kuwa familia ya ‘Kardashians’ haikumpa umaarufu kama watu wanavyofikiria bali umaarufu aliutafuta kwa nguvu zake mwenyewe.

Mrembo huyo aliongeza na kusema kuwa kama kuna mtu ambaye anashika nafasi ya kwanza kwenye list yake basi ni Rapper Drake kwasababu ana asilimia zake za kumfanya afike hapo alipo kwa sasa lakini sio familia ya Kardashians.

“Nilikuwa maarufu hata kabla sijajihusisha na familia ya Kardashians, kuna watu walinikutanisha na Drake na ndipo hapo nilipoanza kufanya kazi za video vixen kwenye nyimbo za wasanii na kuwa model kwenye majarida”

Blac Chyna aliwahi kutajwa kwenye ngoma ya Drake ‘Miss Me’ aliowahi kuuachia mwaka 2010 na aliwahi kuwa mpenzi wa Robert Kardashian na kubahatika kupata nae mtoto mmoja wa kike aitwae Dream.

EXCLUSIVE: Baba wa Masogange anategemewa kuzindua Movie aliyoshiriki Mwanae

Soma na hizi

Tupia Comments