AyoTV

Azam FC hawakujali kama ni Yanga B wala nini

on

Michuano ya Mapinduzi Cup 2019 inaendelea visiwani Zanzibar kwa timu mbalimbali kumenyana, leo ilikuwa ni zamu ya game za Kundi B ambapo Azam FC ambao wapo nafasi ya pili katika Ligi Kuu ya Tanzania bara na Yanga SC wanaongoza Ligi hiyo, waliingia uwanjani kucheza game yao ya Kundi hilo.

Licha ya kikosi cha Yanga SC kutawaliwa na wachezaji vijana kutoka team B, Azam FC hawakuchukulia pouwa na kupanga kikosi chao full music kamili na kushusha kipigo cha magoli 3-o, magoli ya Azam FC yakifungwa na Obrey Chirwa aliyefunga mawili na Enock Atta.

Matokeo hayo yameifanya Azam FC kuwa na point nne wakati Yanga wao wana point tatu pekee, hivyo watahitaji ushindi katika game yao dhidi ya Malindi wakiwa wamesalia na game mbili ili waingie hatua ya nusu fainali, unaweza kutazama magoli yote ilivyokuwa hapa.

Baraka Mpenja wa Azam TV “Walitaka kuandika barua nisitangaze mechi zao”

Soma na hizi

Tupia Comments