Tangaza Hapa Ad

Ukweli kuhusu tetesi za mbunge aliyejiuzulu kupigwa risasi Kilimanjaro


Ni taarifa kutokea mkoani Kilimanjaro ambapo leo December 14, 2017  Kamanda wa polisi Hamis Issah anakanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai aliyekuwa mbunge wa Siha Dr. Godwin Molel amepigwa risasi sita na watu wasiojulikana baada ya kutangaza kujiuzulu ubunge na kumuunga mkono JPM.

Kamanda Hamis amesema taarifa hizo sio za kweli  “tukio la mtu kuuawa sio tukio dogo, mtu kama huyu alikuwa Mbunge na amechaguliwa na wananchi halafu atauawa tu kienyeji na taarifa zisitufikie!, taarifa hizo kwetu hazipo, taarifa za kumtakia mwenzenu kifo sio sawasawa, sheria za mitandao ziwe kali zaidi hata mtu akikosea kidogo akamatwe,” – Kamanda Hamis Issah

“WANASEMA VYUMA VIMEBANA, WEKA GRISI” – JPM, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA

“HII SIO SERIKALI YA UJANJAUJANJA NA MADILI” -WAZIRI NCHEMBA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA

Soma na hizi

Tupia Comments

On AIRSIKILIZA

Usipitwe na hizi

Advertisement