Habari za Mastaa

Mtuhumiwa wa nne wa mauaji ya XXXTENTACION akamatwa

on

Kutokea Marekani taarifa zinaripoti kuwa mtuhumiwa wa mwisho ambaye anakamilisha list ya watuhumiwa  wanne wa mauaji ya rappa marehemu XXXtentacion yaliyofanyika June 18,2018 amekamatwa na polisi wa Broward mjini Florida jana August 7,2018.

Mtuhumiwa huyo anafahamika kwa jina la Trayvon Newsome mwenye umri wa miaka 20 na huku taarifa nyingine kutoka kwa polisi zinadai kuwa amesomewa mashtaka mawili tayari na mahakama ikiwemo kufyatua risasi siku ya tukio hilo na kusababisha mauaji ya rappa huyo na shtaka la pili ni matumizi ya silaha bila kibali.

Mtuhumiwa Trayvon  anaambatana na watuhumiwa wengine watatu ambao ni Michael Boatwright,Dedrick Williams na Robert Allen ambao tayari walikamatwa na wapo ndani wakifanyiwa uchunguzi zaidi kuhusiana na kesi zinazowakabili.

BABA LEVO: “Wanawake elfu saba wananitaka, Watoto watano wana Mama tofauti,”

 

Soma na hizi

Tupia Comments