Premier Bet

Habari za Mastaa

Mwanafunzi atunza fedha kwa miaka miwili ili amsaidie rafiki yake

on

Mwanafunzi Tanner Wilson wa Caddo Hills High School nchini Marekani amepokea sifa baada kutunza fedha zake kwa miaka miwili ili aweze kumnunulia rafiki yake Brandon Qualls wheelchair ya kielektroniki baada ya kujihusisha na kazi za muda mfupi.

Inaelezwa kuwa Brandon Qualls alikuwa akitumia wheelchair ya kujisukuma kwa mikono kwa miaka mingi kutokana na ugonjwa unaomsumbua na kudai kuwa alikuwa akichoka sana mikono mara nyingi na kuelezwa kuwa mwalimu wa Tanner Wilson amesema kuwa mwanafunzi huyo anapenda kujitoa kwa ajili ya watu wengine.

“Mikono yangu ilikuwa inachoka sana na ilinilazimu niwe napumzika, usikate tamaa na Tanner Wilson  husaidia watu kila siku, ni rafiki mzuri sana kwangu” >>>Brandon Qualls

VIDEO: MC PILIPILI AMEJIBU ISHU YA MPENZI WAKE KUDAIWA MJAMZITO

Soma na hizi

Tupia Comments