Tangaza Hapa Ad

Mix

Mrembo wa dunia wa Miss Universe ametangazwa… Kenya yavunja rekodi

on

Shindano la 65 la kumtafuta Miss Universe limemalizika huko Ufilipino ambapo Mshindi ametangazwa kwamba ni Iris Mittenaere wa Ufaransa huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Haiti kupitia kwa Raquel Pelissier na namba 3 akiwa ni Andrea Tovar wa Colombia.

Mshindi wa 2017 baada ya kuvishwa taji

Lilikua ni shindano lenye msisimko hasa ukizingatia Afrika ikiwemo Tanzania ziliwakilishwa na Warembo wa nchi mbalimbali ambapo hamasa zaidi ya kutaka kujua kitachotokea ilipanda zaidi baada ya Miss Kenya Mary Esther Were kutangazwa kuingia kwenye 9 bora akiwa ni Mrembo pekee wa Afrika kuingia Top 9.

Roho za Waafrika hasa Afrika Mashariki zikawekwa juujuu zaidi baada ya Mrembo huyo wa Kenya kutangazwa kuingia kwenye 6 bora ambapo hata hivyo kwenye 3 bora hakufanikiwa, unaweza kutazama kwenye hii video fupi hapa chini akitangazwa kwenye Top 6.

Tanzania iliwakilishwa na Jihan Dimack

ULIPITWA? Miss Tanzania 2016 Diana amekaa kwenye On AiR with Millard Ayo na kusema na waliosema anasura na ngozi mbaya, bonyeza play hapa chini kumtazama

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement