AyoTV

”Nahitaji maelezo yenu mpaka saa 12 jioni mnipe majibu”- Waziri Mkuu

on

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo June 1 2018 amefanya ziara katika kiwanda cha kutengenezea nguo cha Urafiki na kukuta matatizo mbalimbali likiwemo la kiwanda kutofanya kazi.

Akizungumza na uongozi wa kiwanda hicho Majaliwa ametoa maagizo kwamba wakae chini na wabia wao ambao ni Wachina na ifikapo jioni ya leo wampatie majibu na kama watashindwa waondoke.

Ubia wenu hauna tija, nahitaji maelezo yenu, mkae wewe na yeye na ikiwezekana mimi nikitoka mbaki  mjadiliane jioni saa 12 nipate majibu na muheshimiwa Waziri, wewe  Mkuu wa Mkoa  muongoze mjadala huo na mtoke na maadhimioWaziri Mkuu

Siri imefichuka hii ndio sababu kufichwa Wajumbe Kamati ya Makinikia na Wazungu

Soma na hizi

Tupia Comments