Tangaza Hapa Ad

Michezo

VIDEO: Rekodi ya Ronaldo katika ushindi wa Ureno wa 6-0 dhidi ya Andorra

on

Usiku wa October 7 2016 kuelekea October  8 michezo ya kuwania kufuzu kucheza Kombe la dunia 2018 Urusi kwa upande wa mataifa ya bara la Ulaya iliendelea, Ulaya usiku wa October 7 2016 ilichezwa michezo 9, moja kati ya mchezo uliochezwa ilikuwa ni kati ya timu ya taifa ya Ureno dhidi ya Andorra.

Mchezo huo ambao ulichezwa katika dimba la Estadio do Sport Lisboa, mashabiki walishuhudia ukimalizika kwa Ureno kuibuka na ushindi mnono wa magoli 6-0, ushindi ambao ulinogeshwa kwa nahodha wao Cristian Ronaldo kufunga hat-trick ya 42 katika maisha yake ya soka la ushindani.

noticia-165565-portugal-vs-andorra-2

Magoli ya Ureno yalifungwa na Cristiano Ronaldo dakika ya 2, 4, 47 na 68 hiyo ni baada ya Joao Cancelo kufunga goli la tatu kwa Ureno dakika ya 44 na Andre Valente Silva kufunga goli la mwisho kwa Ureno dakika ya 86 na kuwaacha Andorra wakitoka vichwa chini katika dimba la Estadio do Sport Lisboa.

ALL GOALS: Yanga vs Simba October 1 2016, Full Time 1-1

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement