DSTV

Tangaza Hapa Ad

Top Stories

RC Mongella – “Tukiruhusu mzaha kwenye zoezi la vitambulisho vya taifa tutapata shida”

on

Katika zoezi la kusajili vitambulisho vya taifa kwa wananchi takriban milioni 1.7 wa mkoa wa Mwanza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella ameewaambia wananchi pamoja na viongozi wa mitaa kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola kuhusiana na watu wasio Watanzania wanaotaka kujiandikisha kama raia.

Alieleza kuwa suala la uraia ni suala nyeti la ulinzi na usalama wa nchi, na kwamba ukiwepo mwaya wa kuruhusu mzaha, huko siku za mbele yatatokea matatizo.

Wale wasio Watanzania halisi wana fursa ya kujitaja na kupewa vitambulisho na mamlaka hii hivyo kama wewe sio Mtanzania halisi, usiingie kwenye kuvunja sheria kwa kudanganya kuwa wewe ni Mtanzania kwasababu utaingia kwenye mkono wa sheria.” – RC Mongella

Ulipitwa na hii?Majibu ya Bodi ya Mikopo baada ya Wanafunzi kukusanyika Ofisini kwao

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement