Tangaza Hapa Ad

AyoTV

VIDEO: Baadhi ya wanafunzi UDSM walivyofika wizarani kuwasilisha hoja zao kuhusu mikopo

on

Wakati magazeti ya leo yakitoka na habari iliyosema kuwa wanafunzi wa vyuo 66,000 kukosa mikopo, taarifa hizo zilidai kuwa wanafunzi 88,000 walioomba mikopo kutoka bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu, wengi hawatapata.

Taarifa hizo zilizochapishwa na gazeti la mwananchi la October 20 2016 zimesema kuwa uwezo wa bodi hiyo ni kutoa mikopo kwa wanafunzi 21,500 pekee sawa na asilimia 24 na waliopatiwa hadi sasa ni wanafunzi 11,000 sawa na asilimia 12.

Wakati hayo yakielezwa leo October 20 2016 baadhi ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam wakiongozwa na viongozi wa Serikali ya wanafunzi wa chuo hicho ‘DARUSO’ wamefika Wizara ya elimu wakiwa na hoja kuu mbili, uchache wa majina ya wanuafaika wa mikopo yaliyotoka  mpaka hivi sasa na hoja ya pili ni kuhusu vigezo ambavyo vimetumika kwenye fedha ya kujikimu kwa wanafunzi.

Hata hivyo baada ya kufika wizarani hapo wanafunzi hao wamesema hawakupata nafasi ya kumuona waziri wa elimu lakini wamefikisha hoja zao kwa katibu mkuu wa wizara na ametoa ahadi ya kushughulikia hoja hizo.

ULIKOSA HII YA ‘SCORPION’ KUPANDISHWA KIZIMBANI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement