Tangaza Hapa Ad

Michezo

VIDEO: Licha ya migogoro Yaya Toure kadhihirisha ubora wake ndani ya dakika 80

on

Kocha wa Man City Pep Guardiola leo November 19 2016 aliwashangaza wengi baada ya kumpanga kikosi cha kwanza Yaya Toure ambaye alimuacha nje ya kikosi kutokana na makosa aliyofanya wakala wake Dimtri Seluk ya kuongea na vyombo vya habari huku akimponda Guardiola.

3a8c349900000578-3952556-image-m-53_1479571160887

Toure aliomba msamaha mwanzoni mwa mwezi November kama Guardiola alivyoomba kuwa kama Toure anataka kurudi ni lazima wakala wake aombe msamaha, Toure aliomba msamaha kwa niaba ya wakala wake na leo Guardiola alimpa nafasi ya kucheza tena katika kikosi cha Man City.

3a8c393c00000578-3952556-image-m-50_1479571142270

Kiungo huyo wa kimataifa wa Ivory Coast amerudi leo na kucheza mchezo kati ya Man City dhidi ya Crystal Palace na kufanikiwa kufunga goli 2 katika ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Crystal Palace, Toure alifunga magoli katika dakika ya 39 na dakika ya 83.

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement