Habari za Mastaa

DC Jokate amekubali kuwa mlezi wa SZIFF, Tsh milioni 5 juu !!

on

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo amekubali kuwa mlezi wa Sinema zetu Film Festival SZIFF 2019 ikiwa leo September 25,2018 wamezindua awamu ya pili ya tuzo hizo na kuongeza baadhi ya vipengele na kufikia 24.

Kwenye Exclusive interview na Ayo Tv Jokate Mwegelo ameongelea kuhusiana na wazo alilolitoa  la kutumia sanaa kufikisha ujumbe wa mandhari ya Kisarawe ilivyo kwa jamii nchini kwa kufanya filamu tofauti tofauti.

Jokate Mwegelo amegusua pia kampeni yake ya kutokomeza zero ikiwa amekabidhiwa fedha taslimu Tshs.Mil.5 na Azam Media ili kuchangia kampeni hiyo ikiwa na kuwasaidia wanafunzi waliopo kwenye kambi.

Kitu ambacho Ray Kigosi atamwambia Rais Magufuli siku wakionana

Soma na hizi

Tupia Comments