AyoTV

Alichokiandika Dogo Janja baada ya picha ya mkewe Irene na Tbway kuvuja

on

Moja kati ya stori zinazotrend kwa siku ya leo ya Jumapili ya December 17 2017 ni picha ya kimahaba ya muigiza Irene Uwoya ikimuonesha akiwa na mtangazaji Tbway kitandani, wote tunajua Irene Uwoya kwa sasa ameolewa na Dogo Janja, baada ya kuvuja kwa picha hiyo minong’ono imeanza kuenea kuwa inaweza kuvunja ndoa ya Irene Uwoya na Dogo Janja.

Wakati stori hizo zikiendelea kusambaa katika mitandao ya kijamii, kupitia instagram account yake ya Dogo Janja ameamua kupost picha ya mke wake Irene Uwoya na kuandika maneno haya kipindi hiki ambacho kuna minong’ono kuwa ndoa yao imeyumbishwa kwa picha ya Tbway na Irene Uwoya.

“Sigombani na mke wangu kisa jirani kasema nigombane nae, nitakuja nae maisha club leo kumuimbia wimbo mzuri  wa mapenzi na msisahau kuwa ikifika saa sita leo ni Birthday yake so karibuni tumuimbie pamoja”>>>Dogo Janja

Hayo ndio maneno ya msanii Dogo Janja yanayodaiwa kuwa ameyaandika kwa sababu ya maneno maneno ambayo yamesambaa baada ya picha ya kimahaba ya Tbway na Irene Uwoya kuvujaa, Dogo Janja leo anafanya show Maisha Basement akiwa na Aslay ameahidi kuja na mkewe Irene Uwoya.

Rayvanny apata nafasi nyingine nchini Marekani akiwa na Jason Derulo

Soma na hizi

Tupia Comments