Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

HekaHeka

MSIBA HARUSINI: Bibi Harusi kafariki saa 11 baada ya kuolewa…kisa?

on

Kwenye Leo Tena ya Clouds FM leo August 2, 2017 Mtangazaji Geah Habib ameifikisha Hekaheka iliyotokea Mtoni Kijichi DSM ambako nyumba ya Harusi iligeuka kilioni baada ya mwanamke kuolewa na kufariki saa 11 baadaye.

Tukio hilo linatajwa kutokuwa la kawaida baada ya ndoa kufungwa saa Kumi Alasiri na Bibi Harusi kufariki saa Kumi na Moja Alfajiri huku ikidaiwa kuwa alikuwa na ujauzito wa Miezi Sita.

Inaelezwa kuwa siku ya tukio Bwana Harusi aliwapigia simu ndugu wa mkewe kuwapa taarifa ya kuumwa ghafla mkewe ambapo alikuwa analalamika kuumwa tumbo na kumkimbiza Hospitali usiku huo ambako baadaye alifariki.

Bonyeza Play hapa chini kusikiliza Full Story

HEKAHEKA: DSM isivyoishiwa vituko…hiki kimetokea baada ya mwanamke kutotimiza ahadi

Soma na hizi

Tupia Comments