Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Top Stories

Mark Zuckerberg ameahidi marekebisho haya kwenye facebook mwaka 2018

on

Leo January 5, 2018 Mkurungenzi Mkuu wa Facebook, Mark Zuckerberg ameahidi kufanya marekebisho katika mtandao wa Facebook ikiwa ni  malengo yake binafsi kwa  mwaka 2018.

Katika ujumbe alioutuma kwenye ukurasa wake wa Facebook, amesema kuwa amefanya makosa mengi katika kutekeleza sheria na kuzuia utumiaji mbaya wa mtandao huo

Zuckerberg ni maruufu kwa kujiwekea malengo binafsi kila mwaka tangu 2009. Facebook ilizinduliwa mwaka 2004.

Mtandao wa Facebook umekoselewa kwa kuruhusu matangazo yenye uhusiano na nchi ya Russia wakati wa kinyang’anyiro cha ugombea Urais nchini Marekani.

Zuckerburg amesema  “Kuilinda jamii yetu dhidi ya unyanyasaji na chuki, dhidi ya mataifa yanayoingia kati ya maswala ya mataifa mengine, na kuhakikisha kwamba muda unaotumiwa kwenye Facebook unatumiwa vizuri.”

“Hatutaweza kuzuia makosa yote au unyanyasaji wote, lakini kwa sasa tumefanya makosa mengi katika kutekeleza kanuni zetu na kuzuia utumiaji mbaya. Kama tutafanikiwa mwaka huu, basi tutaimaliza mwaka 2018 kwa muelekeo mzuri”” -Zuckerberg

 

Soma na hizi

Tupia Comments