Tangaza Hapa Ad

Mix

Kingine kizuri kutoka Vodacom kupitia promosheni ya banduka kijanja

on

Baada ya kufanya gulio kwa wiki iliyopita ambapo simu  ziliuzwa kwa bei nafuu kabisa mtu wangu,  Kampuni ya simu za mkononi chini ya Vodacom Tanzania  bado inaendelea kuwawezesha watanzania kumiliki simu imara kwa bei nafuu kwa kuendelea na gulio katika maduka yao.

free-device

Taarifa iliyotolewa ni kwamba simu ambazo zinapatikana katika maduka hayo ni pamoja na Smart 7, SmartKicka, Tecno, Itel na Huawei. Mtu wangu ukifika dukani kwa ajili ya kununua simu mojawapo ya simu hizi utatakiwa kununua kifurushi tu na baada ya hapo utapatiwa simu ya kijanja na orijino kulingana na kifurushi alichonunua. Kwa mfano ukinunua kifurushi chenye dakika 1,400, SMS 10,000 na 5GB za intaneti utapewa Smart 7 BURE kabisa.

Vodacom wanakujulisha kwamba simu zote hizo zitakuwa zimeunganishwa na intaneti ambapo mitandao kama Facebook, Twitter, WhatsApp, Snapchat na Instagram zitakuwa tayari zimeshaingizwa kwenye simu hizo, lakini pia unaweza kutembelea kurasa za Vodacom Tanzania za mitandao ya kijamii kufahamu zaidi au duka la Vodacom lililo karibu yako.

 

ULIKOSA VODACOM WALIVYOKABIDHI MIL 20 KWA MSHINDI WA PROMOSHENI YA KAMATA MPUNGA? UNAWEZA KUIANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement