Tangaza Hapa Ad

Mix

Vodacom Tanzania wamezitenga mil 300 kwa ajili ya wateja wake

on

Mtu wangu unaambiwa Vodacom Tanzania wakishirikiana na Benki ya CBA walizindua promosheni kubwa inayojulikana kama “Jiongeze na M- Pawa’‘ ambayo inawawezesha watumiaji wa huduma ya M-Pawa kujishindia zawadi ya fedha taslimu.

Jumla ya shilingi milioni 300 zimetengwa kwa ajili ya promosheni hiyo na mshindi mmoja wa droo kubwa atajishindia kitita cha shilingi milioni 100 na washindi wa wiki watazawadiwa shilingi milioni 20 na washindi wa siku watazawadiwa shilingi milioni moja.

Promosheni hiyo ambayo ilianza mwanzoni mwa mwezi wa 9 itadumu kwa kipindi cha wiki sita na itafikia kilele mwishoni mwa Mwezi Oktober, 2016.

Sasa Vodacom wamechezesha droo ya pili ya wiki iliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo mkazi wa Arusha  Isaack Pilemon alijishindia kitita cha shilingi Milioni 20. Hadi sasa  washindi 2,800 wameongezea mara mbili ya akiba zao za M-Pawa washindi 14 wameshinda milioni 1 kila mmoja na washindi 2 wamejishindia milioni 20  mshindi wa jumla wa shilingi milioni 100 atapatikana mwezi wa October.

unnamed-1

Meneja masoko Huduma za kifedha wa Vodacom Tanzania, Noel Mazoya ‘katikati’, kushoto ni Meneja  wa Huduma za M-Pawa wa Benki ya CBA Eric Luyangi  na Msimamizi wa bodi ya michezo ya Kubahatisha nchini Bakari Maggid.

ULIKOSA HII YA VODACOM KUKABIDHI MIL 20 KWA MSHINDI WA PROMOSHENI YA KAMATA MPUNGA? UNAWEZA KUIANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement