Tangaza Hapa Ad

Mix

PICHA 6: Eneo linalodaiwa kuwepo kwa volcano Kagera, mtaalamu asema ni moto wa kawaida

on

Leo October 6 2016 imeripotiwa habari ikitokea eneo la Katarabuga, kata ya Bwanjai wilaya ya Misenyi Kagera ambapo wananchi wa bonde la Katarabuga wamepatwa na taharuki baada ya kuibuka moto ardhini wakidhani volcano. Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) Prof. Abdulkarim Mruma  amesema moto huo ni wa kawaida tu hivyo wananchi wasiwe na taharuki yoyote.

Prof. Mruma  akitoa ufafanuzi juu ya uvumi huo amesema moto huo ni wa kawaida na kwamba unatokea kwenye ardhi ambayo ina uozo wa majani mengi na yale majani yakiungua yanatoa kitu kama hicho. Prof. Mruma  ameongeza kuwa moto wa namna hii mara nyingi unatokea kwenye makaa ya mawe mtu anapita anaangusha moto mkaa unalipuka panaanza kuungua na ardhi inachubukachubuka kama ilivyotokea kwenye ebneo hilo.

SONY DSC

07 04

SONY DSC

1425671425670

(Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba)

ILIKUPITA HII TAARIFA YA WANANCHI KAGERA KUTAHARUKI BAADA YA KUTOKEA MOTO ARDHINI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement