Tangaza Hapa Ad

Michezo

Vitu vitatu vya kufahamu kabla ya mchezo wa Ndanda FC vs Yanga kuchezwa

on

Ligi Kuu soka Tanzania bara inaendelea tena leo September 7 2016 kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja mbalimbali Tanzania bara miongoni mwa michezo itakayochezwa leo ni pamoja na Ndanda FC watawakaribisha Yanga katika uwanja wa Nangwanda Sijaona kucheza mchezo wao tatu wakati huu utakuwa mchezo wa pili kwa Yanga.

1- Kabla ya mchezo wa leo kuchezwa Yanga na Ndanda FC wamekutana mara 4 katika michezo ya Ligi Kuu, huku mchezo mmoja pekee ndio umewahi kuchezwa katika uwanja wa Nangwanda na Yanga alifungwa goli 1-0, wakati mchezo mmoja Yanga ndio kawahi kumfunga Ndanda FC na michezo miwili wametoka sare.

IMG_0143

2- Baada ya kuichezea klabu ya Dar es Salaam Young Africans kwa misimu sita, kiungo Salum Telela ndio atakuwa anacheza kwa mara ya kwanza dhidi ya Yanga toka aachwe na klabu hiyo katikati ya mwaka 2016.

3- Yanga imecheza mechi moja msimu huu wa 2016/2017 na kufanikiwa kuifunga African Lyon kwa goli 3-0, ila kwa Ndanda FC huu utakuwa mchezo wake wa tatu msimu huu wa kwanza kucheza katika uwanja wake wa nyumbani baada ya kupoteza michezo miwili ya awali dhidi ya Mtibwa Sugar kufungwa goli 2-1 na Simba kufungwa goli 3-1.

GOAL AND HIGHLIGHTS: YANGA VS TP MAZEMBE JUNE 28 2016, FULL TIME 0-1

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement