Tangaza Hapa Ad

Michezo

Yanga wameanza kutetea Ubingwa wao wa VPL kwa ushindi

on

Ligi Kuu soka Tanzania bara leo August 28 2016 imeendelea kama kawaida kwa bingwa mtetezi wa michuano hiyo klabu ya Dar es Salaam Young Africans kucheza mchezo wake wa ufunguzi dhidi ya African Lyon katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

IMG_0056

Huu ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa Yanga katika msimu wa 2016/2017 wakati African Lyon huu ni mchezo wa pili toka wapande Ligi Kuu msimu huu baada ya kushuka daraja misimu kadhaa nyuma, katika mchezo huo Yanga ambao ni Mabingwa watetezi wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 3-0.

IMG_0071

Magoli ya Yanga yalifungwa na Deus Kaseke dakika ya 19 na Simon Msuva dakika ya 60 kipindi cha pili, baada ya hapo kocha wa Yanga Hans van Pluijm alifanya mabadiliko ya kumtoa Simon Msuva na kumuingiza Juma Mahadhi aliyeenda kupachika goli la tatu dakika za nyongeza, hilo linakuwa goli la kwanza la Mahadhi toka ajiunge na Yanga.

Matokeo ya mechi nyingine za VPL zilizochezwa leo August 28 2016

  • Toto Africans 0-1 Mbeya City

GOAL AND HIGHLIGHTS: YANGA VS TP MAZEMBE JUNE 28 2016, FULL TIME 0-1

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement