Kutoka kwenye ukurasa rasmi wa Adam Mchovu leo August 16,2020 staa mtangazaji ameomba radhi kutokana na tukio lililotokea jana katika Uwanja wa Uhuru la yeye kumpiga teke Muimbaji Emmanuel Mbasha.
‘‘kwanza nimuombe radhi Rais wetu wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, pili kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuniamini na kunipa nafasi ambayo bahati mbaya ilitokea tukapishana kauli jukwaani na Msanii mwenzangu” Adam
“Nimepokea simu mbalimbali za Viongozi wa Serikali wakinifahamisha namna nilipaswa kufanya wakati wa shambulio lile la mimi kuitwa ‘ADAM Unajua we ni Bangi sana’ Kwa pamoja nimewaelewa” Adam
“Nikutake radhi pia Emmanuel Mbasha Mimi sina tatizo lolote binafsi na Wewe kilichotokea ni kukwazika na kauli yako uliyotoa dhidi yangu kwenye tukio kubwa la Kitaifa lililotazamwa na Mamilion ya Watanzania” Adam
“Sisi wote Vijana kuna muda tunakosea na tunawekana sawa japo njia zingine si nzuri. Asante kwa Jeshi la Polisi chini ya IGP Simon Sirro kwa maelekezo yenu. Nitayatii na kwa sasa mimi ni Balozi wenu wa hiari kabisa” Adam