Top Stories

“Tumechoka, Rais amekataa, mmoja wenu tutamtoa mfano”-Naibu Kijaji (+video)

on

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Ashatu Kijaji ameasema kuwa kumekuwa na viashiria vingi vya matukio ya rushwa katika baadhi ya Sekta zilizopo chini ya Wizara hiyo ikiwemo sekta ya manunuzi na kusababisha hasara kwa Taifa ambapo ameahidi kuwashugulikia wahusika wote ikiwemo kuwafukuza kazi.

“Kama Taifa tumechoka kupeleka fedha za Umma alafu hatuoni matokeo sahihi kwenye utekelezaji wa miradi, Wananchi wamechoka na Rais Magufuli alishakataa kuchoka na anasema atashugulika na kila mmoja anayesababisha tuwe hapa na tutatoa mfano kwa mmoja wenu ili sote tujue umuhimu wa utekelezaji wa sheria” Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Ashatu Kijaji

‘BUSTANI YA MUNGU’ INA MAUA 40 HAYAPATIKANI POPOTE DUNIANI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

Soma na hizi

Tupia Comments