Tangaza Hapa Ad

Michezo

Taarifa ambazo ni pigo kwa mashabiki wa Arsenal na kocha Wenger

on

Ni kweli taarifa zilizotolewa leo na klabu ya Arsenal haziwezi kuwapa furaha mashabiki wa Arsenal na kocha wao Arsene Wenger, ukizingatia wakati huu ambao watakuwa na mtihani mzito wa kurudisha heshima katika Ligi Kuu England.

Arsenal leo October 26 2016 wamepokea taarifa mbaya kuhusu mshambauliaji wao raia wa Hispania Lucas Perez kuwa atakaa nje ya uwanja kwa wiki sita hadi 8 kufuatia jeraha lake la enka alilolipata katika mchezo wa EFL Cup dhidi ya Reading uliomalizika kwa Arsenal kupata ushindi wa goli 2-0 siku ya Jumanne ya October 25 2016.

lucas-perez-710735

Lucas Perez

Perez alitolewa nje ya uwanja dakika ya 72 ya mchezo baada ya kuumizwa na Danzell Gravenberch wa Reading, kocha wa Arsenal Arsene Wenger ameoneshwa kuchukizwa kupita kawaida kiasi cha kuita rafu aliochezewa Perez na Danzell Gravenberch ni “Rafu ya kipumbavu aliochezewa mshambuliaji wa Arsenal itakayomuweka nje wiki 8”

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement