Tangaza Hapa Ad

BreakingNews

BREAKING: Maamuzi ya Mahakama kuhusu dhamana ya Wema Sepetu

on

Leo kwenye Mahakama ya hakimu mkazi kisutu Dar es salaam alifikishwa Mwigizaji Wema Sepetu ambaye kuanzia wiki iliyopita alikua akishikiliwa na jeshi la Polisi kwenye sakata la dawa za kulevya.

Mahakamani Kisutu leo imekubali kutoa dhamana ya mwigizaji huyo ambapo imehusu Wadhamini wawili na milioni 5 ambapo pia tarehe 22 mwezi huu anarudi tena Mahakamani kusikiliza majibu ya Mkemia Mkuu wa Serikali kujua kama ni mtumiaji wa dawa za kulevya.

Hakimu pia alimwambia Mwendesha mashtaka alete hilo jibu la Mkemia mkuu mapema iwezekanavyo, endelea kukaa karibu na millardayo.com kupitia APP ya Millard Ayo kwenye Android na IOS, pia FB Twitter na Instagram kwa jina hilohilo la @millardayo taarifa zaidi zitakujia.

VIDEO: Wema Sepetu alivyopokelewa Dar baada ya kuukosa Ubunge wa viti maalum

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement