Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Sauti ya Wema Sepetu iliyosambaa akiwatoa mashabiki hofu

on

Mwigizaji wa Tanzania Wema Sepetu ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita alifika kwenye kituo kikuu cha Polisi kati Dar es salaam baada ya kutajwa kwenye list ya wanaotuhumiwa kwenye utumiaji na biashara ya dawa za kulevya, amewatoa hofu Mashabiki zake.

Wema amesikika kwenye sauti aliyoiweka kwenye mitandao na hapa ninamnukuu anachokisema >>> ‘Nadhani natakiwa kusema kitu sababu najua nina mashabiki, nina watu wananipenda na kunifatilia…. nina watu wanani-support, nina watu wana hofu kuhusu mimi’

Nina watu ambao wananijali sana na nina uhakika yani wana wasiwasi sana lakini nataka tu niwaambia kwamba msiwe na wasiwasi‘ – Wema Sepetu 

Sauti yenyewe unaweza kuisikiliza kwa kubonyeza play hapa chini au kwa urefu ukaipata kwa ku-download APP ya Wema Sepetu kwenye Google Store kupata habari zake zote zinazomuhusu.

Unaweza kuisikiliza sauti hii fupi kwa kubonyeza play hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement