DSTV


Tangaza Hapa Ad

Top Stories

SHAHIDI: “Nashangaa kusikia Manji anatumia Dawa za Kulevya”

on

Jumanne, September 26, 2017 Kesi ya dawa za kulevya inayomkabili Mfanyabiashara Yusuf Manji imeendelea kwa siku ya pili kati ya tatu za kusikiliza ushahidi mfululizo ambapo leo umetolewa ushahidi wa mashahidi watatu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Katika kesi hiyo, shahidi wa tano, Maria Rugalabumu (63) amemueleza Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha kuwa yeye ni Sektretari wa Manji (Katibu Muktasi) na Ofisi ya Quality Group Ltd.

Akiongozwa na Wakili wa utetezi Hajra Mungula, amedai kuwa anafanya kazi katika kampuni hiyo tangu mwaka 1994 hadi sasa, wakati huo Manji akiwa anasoma.

Alipoulizwa na Wakili Mungula kwamba anamfahamu vipi Manji, amesema anamfahamu tangu anasoma na kwenye masuala ya kazi anamfahamu tangu 1997 baada ya kurithi mikoba ya baba yake.

Pia alipoulizwa kama kuna vitu vya Manji huwa anavitunza, akajibu ndio ambapo miongoni mwa vitu anavyomtunzia ni Sigara.

Aidha, amedai kuwa anashangazwa kusikia kuwa Manji anatumia dawa za kulevya hali ya kuwa amemfahamu takribani miaka 19 akisema kuwa majukumu yake ni uangalizi wa ofisi yake na ya Manji, pia kuchapa barua, kupokea wageni na kutuma barua zinazotoka ofisi yao na kusema kuwa Manji ni mchapakazi na anaweza kufanya kazi kwa muda mrefu na huwa anapenda kazi zake.

Shahidi huyo, amedai kuwa amemfahamu tangu Manji anasoma Chuo, pia alivyoanza kufanya kazi kwa Baba yake na kuieleza Mahakama kwamba yeye ndiye aliyetoa kopi ya nakala ya dawa za Manji kutoka kwa Dokta wake Marekani.

Nakala hiyo aliipata kwa njia ya e-mail, ambapo baada ya kuitoa nakala alimpatia askari ili ampe Manji ambaye alilazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, hivyo anaomba Mahakama ipokee kama sehemu ya kielelezo.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali Mkuu, Timony Vitalis alipinga kupokelewa kwa barua hiyo kwa sababu haina uthibitisho wa kiuhalisia na daktari aliyeituma.

Baada ya kueleza hayo Hakimu Mkeha alitoa uamuzi ambapo alikubaliana na Wakili Vitalis, ambapo alisema Mahakama haiwezi kupokea kielelezo hicho.

KESI YA MANJI: “Moyo wa Manji umewekwa vyuma kumsaidia kupumua” – Shahidi

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement