Tangaza Hapa Ad

Michezo

FULL TIME: Matokeo yote mechi za EPL zilizochezwa jioni ya leo

on

Kabla ya mchezo wa baadaye leo ambao utazikutanisha Leicester City ambao watakuwa nyumbani King Power Stadium kuwakaribisha Liverpool, mechi saba zimepigwa katika viwanja saba tofauti kwenye Ligi Kuu ya England, maarufu kama EPL.

Katika mechi hizo, Chelsea wamefanikiwa kupata ushindi wa mabao 4-0 wakiwa ugenini dhidi ya Stoke City mabao yakifungwa na Alvaro Morata aliyefunga Hat-trick na Pedro. Manchester City ikiwa nyumbani Etihad imeshinda mabao 5-0 dhidi ya Crystal Palace mabao ya City yakifungwa na Sané dakika ya 44Sterling dakika za 51 na 59Agüero dakika ya 79 na Delph katika dakika ya 89.

Mchezo mwingine ulikuwa kati ya Everton iliyoshinda mabao 2-1 dhidi ya Bournemouth wakati bao pekee la Lukaku likiipa ushindi Manchester United ugenini dhidi ya Southermpton. Swansea City wakalala nyumbani kwa mabao 2-1 dhidi ya Watford, Burnley na Huddersfield zikatoka sare ya 0-0 huku mchezo wa awali ukizikutanisha West Ham United waliokubali kipigo cha mabao 3-2 kutoka kwa Tottenham.

MAGOLI YOTE: Mbao FC vs Simba FC September 21 Mwanza (2-2)

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement