DSTV


Tangaza Hapa Ad

Michezo

FULL TIME: Matokeo yote mechi zilizochezwa jioni hii PREMIER LEAGUE

on

Manchester United imeendelea kufanya vizuri katika mechi za Ligi Kuu England maarufu kama EPL baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Crystal Palace ambayo imepoteza michezo yote saba ya Premier League msimu huu bila hata kufunga bao.

Mabao ya United ambayo haijapoteza mchezo hata mmoja hadi sasa, yamefungwa na Juan Mata, Marouane Fellaini aliyefunga mara mbili na Romelu Lukaku.

Katika michezo mingine, FC Bournemouth imetoka sare ya 0-0 na Leicester City wakati Stoke City ikiichapa Southampton mabao 2-1 mabao ya wenyeji yakifungwa na Mame Biram Diouf na Peter Crouch huku bao la Southampton likifungwa na Maya Yoshida.

Richarlison alifunga bao la kusawazisha dakika za lala salama Watford ikitoka nyuma na kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya West Bromwich Albion ambayo ilipata mabao mawili ndani ya dakika tatu yakifungwa na Salomon Rondon na Jonny Evans, lakini Abdoulaye Doucoure akapunguza.

West Ham imefanikiwa kutoka mkiani mwa Premier League baada ya bao pekee la Diafra Sakho kuipa ushindi dhidi ya Swansea.

Katika mchezo wa mapema kabisa, Tottenham ilipata ushindi wa mabao 4-0 ugenini dhidi ya Huddersfield huku mabao yao yakifungwa na Kane aliyefunga mara mbili, Davies na Sissoko.

 MAGOLI YOTE: Mbao FC vs Simba FC September 21 Mwanza (2-2)

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement