Michezo

Alichopanga kufanya Tyson Fury baada ya pambano na Wilder

on

Bondia muingereza Tyson Fury aliyeingia kwenye headlines baada ya kutoka sare na bondia Wilder katika pambano la uzito wa juu lililochezwa alfajiri ya December 2 2018, pambano lenye round 12.

Fury anaingia kwenye headlines baada ya kutangaza kuwa sehemu ya pesa zake alizozipata katika pambano lake dhidi ya Wilder, lilomalizika kwa mabondia hao kutoka droo, atatoa msaada pesa hizo ila wengi wanaamini kuwa bondia huyo alistahili ushindi kwani alitawala pambano kuanzia mwanzo mwisho.

Tyson Fury

Tyson Fury amepanga kutoa pound milioni 8 ambazo ni zaidi ya Bilioni 23.3 za kitanzania kwa watu masikini na kuwajengea makazi baadhi ya watu wasiokuwa na makazi, hiyo ikiwa ni sehemu ya kuamua kurudisha fadhila kwa jamii.

EXCLUSIVE: Kauli ya Singida United kushindwa kulipa wachezaji, mbona wanasajili?

Soma na hizi

Tupia Comments