PremierBet Tanzania Usain Bonus Ad

Michezo

Japokuwa hajatajwa, Messi atahudhuria tuzo za FIFA Sept 24

on

Baada ya nahodha wa timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo kukosekana katika sherehe za utoaji wa tuzo za mchezaji bora wa Ulaya (UEFA) msimu wa 2017/2018, wengi walikuwa na hamu ya kutaka kujua kama Messi atahudhuria tuzo za FIFA Jumatatu ya September 24 2018.

FIFA walitangaza majina matatu ya wachezaji Cristiano Ronaldo wa Juventus, Luca Modric wa Real Madrid na Mohamed Salah wa Liverpool kuwa ndio wamefanikiwa kuingia TOP 3, hivyo Messi ndio kwa mara ya kwanza atahudhuria tuzo hizo kama mtazamaji na sio mshindani.

Lionel Messi ambaye ni mshindi wa tuzo tano za Ballon d’Or katika msimu wa 2017/2018 hakuwa na msimu mzuri ila Messi yupo katika wachezaji wanaowania tuzo ya goli bora na kikosi bora hivyo kuna uwezekano wa kushinda nafasi hizo pia.

Takwimu za Ronaldo, Messi, MO Salah na Modric wakiwa na vilabu vyao msimu huu.

EXCLUSIVE: Licha ya kuwa na pesa na ustaa, hii ndio Sababu inayomfanya Samatta asiringe

Soma na hizi

Tupia Comments