PremierBet Tanzania Usain Bonus Ad

Michezo

Waziri Mwakyembe awaomba Watanzania, tutafungwa Cape Verde

on

Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Dr Harrison Mwakyembe Jumatano ya October 3 2018, amewaomba watanzania wote kuinuka na kuiunga mkono timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ili ifanikiwe.

Dr Mwakyembe ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari kuwa watanzania wanapaswa kujitolea na kukata tiketi ya kwenda Cape Verde na ndege maalum ili kuwawezesha wachezaji wa Taifa Stars wasichoke kuelekea mchezo huo wa ugenini na ule wa nyumbani.

Taifa Stars kwa sasa inajiandaa kwenda kucheza mchezo wake wa tatu wa kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika kwa mwaka 2019 nchini Cameroon dhidi ya Caper Verde October 12 na baadae kurudiana October 16 jijini Dar es Salaam.

Kutokana na ratiba hiyo kuwa ngumu ATCL imetoa ndege aina ya Dream Liner watanzania wanapaswa kuchangia kwa kukata tiketi za kwenda kuagngalia game hiyo, kutokana na kukosa ndege ya moja kwa moja itakkayowawezesha kuwapeleka na kuwarudisha katika mchezo wa marudiano.

“Simba tumewaachia, sisi hatuna presha”-Kocha wa Yanga

Soma na hizi

Tupia Comments