Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Ulishawahi kufahamu hili la kusikitisha kuhusu Shakira?

on

Staa maarufu kutokea Colombia Shakira ambaye alitamba na ngoma zake kali zikiwemo nyimbo kama  ‘Wakawaka’, Hips don’t lie , Whenever na nyingine nyingi ambazo zilimpatia umaarufu mkubwa duniani.

Katika mahojiano aliyoyafanya na Sunday Mirror alikiambia chombo hicho  kuwa alikuwa na ndoto kubwa  za kuwa mwanamuziki mkubwa alivyokuwa mdogo lakini ndoto hizo zilikuwa zikijaribu kuzimwa na mwalimu wa kwaya shuleni kwao na kumwambia kuwa hawezi kuimba bali anaimba kama mbuzi.

Maneno hayo yalimuumiza sana lakini pia yalimpa nguvu na kufanya mazoezi zaidi katika uimbaji wake  hadi kutimiza ndoto yake na kufikia kupata tuzo mbalimbali kama MTV music award Best choreography 2006, Wimbo bora wa mwaka katika tuzo za Grammy 2016 , Best Female artist MTV Europe Music Award 2005 na nyingine nyingi.

Kwa sasa Shakira ameolewa na mchezaji mpira Gerard Pique anayechezea timu  ya Barcelona na wamefanikiwa kupata watoto wawili.

Wimbo uliomfanya ‘Sam wa Ukweli’ ‘afie studio’ WALIMWENGU

Soma na hizi

Tupia Comments