PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Habari za Mastaa

Esha Buheti “nawaza mengi mpaka nakufuru Mungu, picha ya ajali hainitoki”

on

Taarifa za kifo cha mtoto wa aliyekuwa muigizaji wa Bongo Movie Munalove  aliyefariki July 3,2018 Nairobi Kenya zimeonekana kuwagusa wengi kutokana na umri aliokuwa nao Patrick na hivyo mastaa mbalimbali kupost kuhusiana na taarifa hizo kupitia mitandao ya kijamii.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Esha Buheti ameelezea jinsi alivyoguswa na taarifa hizo ikiwemo na kuelezea tukio lake la kunusurika katika ajali aliyoipata usiku wake na kuwaza mengi kuhusiana na kifo cha mtoto huyo.

Kupitia instagram account ya Esha Buheti ameandika “Huyu mtoto ananifanya nawaza mambo mengi sana mpk nakufuru yarrab…..Kwanini tunapata furaha kisha inageuka kua huzuni? Jana nimepata ajali ya gari wakati narudi nyumbani usiku nikitokea kazini azam….lori iliacha njiaa ikanifata kwenye gari yangu…ikanibana upande wa dereva…nililia sana nikawaza je ningekufa jana palepale inamaana ndo ningeacha wanangu?”

“Sijalala naweweseka usiku kucha ile picha ya ajali hainitoki akili…..hiyo ni ajali tuu jee Muna alopoteza mwanae ambae hatomuona tena? Anaumiajee?”

“EEH MUNGU TULINDIE WAPENDWA WETU YARRAB NAWAZA MENGI MASKINI MWANANGU BADO MDOGO HATA ASINGEELEWA KITU KAZI INGEKUA KWA CLARISSA WANGU KUMWAMBIA MAMA AMEFARIKI KWENYE AJALI….KICHWANI NAWAZA MENGI MUNGU WANGU ASANTE KWA KUNITOA SALAMA KWENYE HILI BALAAH….SIWEZI SAHAU….😢😢😢😢”

Dj Vasley aliyepata mafanikio kupitia Davido kumtumia kwenye Show zake

Soma na hizi

Tupia Comments