AyoTV

Bondia Hassan Mwakinyo kapata dili la ubalozi mbele ya Waziri Mwakyembe

on

Bondia Hassan Mwakinyo baada ya kufanikiwa kufanya vizuri katika mchezo wa ngumi hivi karibuni, leo amepata dili la miaka mitatu la kuwa balozi wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa.

Mwakinyo atapata fursa ya kupata vifaa na vitu vyote muhimu vya michezo ya ubondia kutoka SportPesa, Mwakinyo amesaini mkataba huo akiwa mbele ya waziri wa habari, utamaduni sanaa na michezo Dr Harrison Mwakyembe na Mkurugenzi Utawala na Utekelezaji wa SportPesa Abbas Tarimba.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri bondia Hassan Mwakinyo alijizolea umaarufu mkubwa mwezi September 2018 baada ya kumpiga bondia muingereza Sam Eggington kwa kumpiga Technical Knock Out  round ya 2 katika pambano la round 10.

“Tumeshinda ili kuweka tabasamu usoni kwa MO Dewji”-Kocha Simba SC

Soma na hizi

Tupia Comments