PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Michezo

PICHA 8: Licha ya kutolewa World Cup na vitisho, haya ndio mapokezi ya Colombia

on

Timu ya taifa ya Colombia baada ya kutolewa katika fainali za Kombe la Dunia 2018 dhidi ya England katika hatua ya 16 bora, wamewasili nchini kwao nchini Colombia katika mji wa Bogota na kupata mapokezi makubwa kutoka kwa wananchi wa Colombia.

Clombia ambao walitoka kwa mikwaju ya penati 4-3 dhidi ya England baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare ya kufungana goli 1-1, wamewasili katika mji mkuu wa nchi hiyo Bogota na kupata mapokezi makubwa kwa kuonesha kuipambania nchi yao hadi dakika ya mwisho.

Pamoja na kuwa iliripotiwa kuwa wachezaji wawili wa Colombia waliokosa penati akiwemo Carlos Bacca walipata meseji za vitisho mtandaoni lakini katika jiji la Bogota mambo yamekuwa tofauti na kila mtu akionekana kuwa na furaha na timu hiyo na kuisapoti.

Haji Manara kapenda usiku wa VPL ila kafunguka wasiwasi wake

Soma na hizi

Tupia Comments