Tangaza Hapa Ad

Michezo

Wachezaji wa Yanga Dida na Kaseke wapatwa na msiba, mmoja kampoteza baba na mwingine babu

on

Siku ya Jumapili ya August 28 2016 haikuwa nzuri kwa golikipa wa klabu ya Dar es Salaam Young Africans Deogratus Munish Dida licha ya kupata ushindi katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya African Lyon.

Dida inaripotiwa kuwa baada ya mchezo kumalizika alipokea taarifa za msiba wa baba yake mzazi ambaye alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kansa kwa muda mrefu na alikuwa kalazwa katika hospitali ya Ocean Road, msiba upo Temeke Mikoroshini.

pluijm rambirambi

Baada ya taarifa hizo kuenea na kumfikia kocha mkuu wa Yanga Hans van Pluijm alitumia ukurasa wake wa facebook kutuma salam za rambirambi kwa golikipa huyo, hata hivyo mchezaji mwingine wa Yanga pia Deus Kaseke amempoteza babu yake siku moja sawa na Dida.

GOAL AND HIGHLIGHTS: YANGA VS TP MAZEMBE JUNE 28 2016, FULL TIME 0-1

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement