Biko Ad
MPTV Ad
TIC Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

CAF imetoa adhabu na mkenya kafungiwa maisha

on

Shirikisho la soka barani Afrika CAF Jumamosi ya July 7 2018 ilikaaa kikao cha maadili na kujadili kuhusiana na mienendo mbalimbali ya marefa ambao wametajwa kwa kashfa mbalimbali.

CAF imekaa na kuamua kutoa adhabu kwa waamuzi na waamuzi wasaidizi 11 ikiwafungia kuchezesha soka katika mechi zote zinazohusika na CAF kwa kipindi cha kuanzia miaka miwili na wengine miaka 10 huku muamuzi msaidizi kutoka Kenya Marwa Range akifungiwa maisha.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Marwa Range alikuwa ni sehemu ya waamuzi wasaidizi ambao wangechezesha game za Kombe la dunia lakini aliondolewa dakika za mwisho na FIFA kufuatia kukumbwa na kashfa ya kupokea rushwa ya dola 600 za kimarekani ambazo ni zaidi Tsh milioni moja ya kitanzania.

Soma na hizi

Tupia Comments