Tangaza Hapa Ad

Michezo

Yanga yashindwa kuvunja rekodi yao dhidi ya Ndanda FC Nangwanda

on

Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea leo September 7 kwa michezo mitatu kupigwa katika viwanja vya Taifa Dar es Salaam, Sokoine Mbeya na uwanja wa Nangwanda Sijaona Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara Dar es Salaam Youg Africans walisafiri wakitokea Dar es Salaam kwenda Mtwara kuwafuata Ndanda FC kwao.

IMG_0015

Hata hivyo Yanga ambao walikuwa wanatarajiwa kukutana na upinzania mkubwa kutoka kwa Ndanda FC kutokana na rekodi ya mechi zao za nyuma, Yanga wamelazimishwa suluhu ya 0-0 baada ya Ndanda kufanikiwa kucheza mchezo wakulinda goli lao kwani kipindi cha pili walicheza nyuma zaidi.

IMG_0209

Huu ni mchezo wa tano kwa Yanga na Ndanda FC kukutana katika Ligi Kuu soka Tanzania bara, lakini ni mara ya pili kwa timu hizo kucheza katika uwanja wa Nangwanda huku Yanga akiwa kafungwa mara moja katika uwanja huo na kutoa suluhu mara moja, kwa ujumla Yanga na Ndanda wamefungana mara moja moja na kutoka sare mara tatu.

IMG_0026

Matokeo ya mechi nyingine za VPL zilizochezwa leo September 7

  • Simba SC 2-1 Ruvu Shooting
  • Tanzania Prisons 0-1 Azam FC

GOAL AND HIGHLIGHTS: YANGA VS TP MAZEMBE JUNE 28 2016, FULL TIME 0-1

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement