PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Habari za Mastaa

Ommy Dimpoz kamjibu Steve Nyerere “Konseksheni Yangu kubwa ni Afya”

on

Siku ya February 9,2019 Mwigizaji Steve Nyerere alitumia ukurasa wake wa instagram kuomba radhi Watanzania pamoja na Ommy Dimpoz kutokana na kauli yake aliyoiongea baada ya Ommy kufanyiwa operesheni ya koo na kusema kuwa hatoimba tena.

Ommy Dimpoz ameamua kukubali na kumsamehe Steve Nyerere na kumsisitiza kuwa binadamu huwa wanakosea hivyo hana kinyongo nae lakini cha muhimu anachokiangalia kwa sasa ni afya yake ili iweze kuimarika zaidi. Ommy Dimpoz amewashukuru mashabiki kwa kufikisha views Mil 1 kwa wimbo wake wa ‘Ni Wewe’ katika mtandao wa YouTube baada kuiachia rasmi Feb 04,2019.

“Thank you for the Love & Support 1 Mil viewers in 4 days kwangu ni wengi sanaaaa ukizingatia December yote ilinikuta Kitandani wala sikuwa na matarajio kama nitasimama tena pia stress na mawazo ukiona wasanii wenzako wako busy na msimu wa Sikukuu kuingiza chochote”

“Lakini nilimshukuru Mungu Maana yeye ndo Anayepanga na Sikuchoka kumuomba Naimani Afya yangu itaendelea kuimarika zaidi na Zaidi Inshaallaah Kuhusu my Brother TIVU AKE 🤣 @stevenyerere2 Mimi kama nilivyosema Mwanzo sina kinyongo na Wewe najua kama binadamu uliteleza na kuna kitu umejifunza”

“Ningependa utambue bado nakuheshimu sana si unajua wewe ndo kiongozi wetu kwenye Mambo yetu yale 😜🤣🤣 sasa hivi Konseksheni Yangu kubwa ni Afya mkubwa mengine tusahau sawa🤣 halafu kuhusu hizi clip niache tu nipost maana zinachekesha halafu ntakuwa nawasapot wachekeshaji wenzako 😂”

HATIMAE STEVE NYERERE AMUOMBA RADHI OMMY DIMPOZ

 

Soma na hizi

Tupia Comments