Habari za Mastaa

Heriet Paul apata shavu tena kwenye onyesho la Victoria Secret

on

Mwanamitindo Heriet Paul azidi kuipeperusha bendera ya Tanzania kimataifa hii ni baaada ya kupata nafasi ya kutembea kwenye jukwaa la maonyesho ya Victoria Secret mwaka huu 2018 kwa mara ya tatu.

Maonyesho hayo ya Victoria Secret yalifanyika December 2,2018 nchini Marekani ambapo Heriet Paul alipata nafasi ya kuungana na Wanamitindo maarufu duniani akiwemo Kendall Jenner, Adrana Lima, Behati, Prinsloo, Gigi and Bella Hadid, Winnie Harlow na wengine wengi.

Heriet Paul amepata mafanikio makubwa kupitia maonyesho hayo ikiwa pamoja na kununua nyumba nchini Marekani na kwa sasa makazi yake yapo nchini humo.

EXCLUSIVE: CHALII YA CHUGA BENEFICIAL KAFUNGUKA “NI HUYO MIMI”

Soma na hizi

Tupia Comments