Tangaza Hapa Ad

AyoTV

AUDIO: Mkwasa amesikitishwa na Kelvin Yondani kutojibu meseji zake wala kupokea simu

on

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars tayari imeondoka Dar es Salaam kuelekea Nigeria kucheza mchezo wake wa mwisho wa kukamilisha ratiba wa michuano ya kufuzu Kombe la mataifa ya Afrika 2017 dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles.

Kulikuwa na taarifa kuwa beki wa kati wa Yanga Kelvin Yondania hajawasili katika kambi ya timu ya taifa licha ya kupigiwa simu mara kadhaa na viongozi na kocha wa timu ya taifa Charles Boniface Mkwasa, afisa habari wa shirikisho la soka Tanzania TFF Alfred Lucas ameeleza kusikitishwa kwa kocha Mkwasa kumkosa Yondani.

“Siwezi kuficha mawazo ya mwalimu toka tunatoka hoteli hadi Airport   kunung’unika kuhusiana na mchezaji Kelvin Yondani kutojibu meseji za mwalimu wala kupokea simu, pengine mnaweza kuhoji TFF tutachukua hatua gani, ukweli tunasubiri ripoti ya mwalimu” >>> Alfred Lucas

GOAL AND HIGHLIGHTS: YANGA VS TP MAZEMBE JUNE 28 2016, FULL TIME 0-1

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement