Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Chance The Rapper akubali kile alichofanya Michael Jackson kwenye jamii

on

Kwa mujibu wa mtandao wa ‘Complex’ umeripoti kuwa Chance The Rapper amemtaja mfalme wa Pop Michael Jackson kama ‘Role Model’ wake kwenye upande wa kusaidia jamii, kwenye mahojiano na Forbes  Chance aliweka wazi kuwa hadi kufika hapa alipo amepata msukumo toka kwa watu kama Kareem Abdul-Jabbar ambaye ni mchezaji wa Basketball wa zamani, Drake na Kanye West.

Chance The Rapper amesisitiza na kusema kuwa Marehemu Michael Jackson amefanya makubwa zaidi kwake, ikiwemo kutoa kwa jamii ndio kikubwa ambacho kimemfunza na kusema kuwa muda mwingi huwa yupo na Kareem na amefanya vitu vingi kwa ajili ya jamii na anaamini Kareem ni mtu mzuri sana.

“Mkubwa kwa muda wote, juu zaidi ya mastaa wote, nafikiri ametoa zaidi ya trilioni 1.3 na zaidi kuisaidia jamii yake. Mtu pekee ambaye naweza kumfikiria linapokuja suala la msaada ni mwanamuziki Michael Jackson.” Alisema Chance The Rapper

VIDEO: MREMBO POSHY AMEJIBU KUDAIWA KUTOKA NA MWANAUME ANAYEDAIWA NI WA ZARI THE BOSS LADY

Soma na hizi

Tupia Comments