Tangaza Hapa Ad

AyoTV

VIDEO: “Sijawahi kushindwa katika maisha yangu labda itokee nikiwa Yanga” Lwandamina

on

Uongozi wa klabu ya Dar es Salaam Young Africans leo November 25 kupitia makamu mwenyekiti wake Frank Sanga, wamemtambulisha rasmi aliyekuwa kocha mkuu wa klabu ya Zesco United ya Zambia George Lwandamina kuwa kocha wao mkuu.

AyoTV baada ya utambulisho mbele ya vyombo vya habari tukampata George Lwandamina katika exclusive interview, kitu gani kimemfanya avutiwe kujiunga na Ligi ya Tanzania hususani Yanga.

“Kupata changamoto mpya unajua maisha hayaendi bila changamoto najua haya mazingira yatanifunza namna ya kukabiliana na vitu vipya katika maisha, Ligi ya Tanzania ni nzuri na ina ushindani mkubwa lakini huwezi kulinganisha na Ligi ya Zambia, Ligi ya Zambia ipo level nyingine”

“Kiukweli kitu pekee kilichonifanya nijiunge na Yanga ni kupata changamoto mpya, unajua sijawahi kufeli katika maisha yangu sijui labda itokee nikiwa Yanga”

VIDEO: Sababu iliyofanya kocha Hans afute uamuzi wake wa kujiuzulu Yanga 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement