Michezo

“Watoto kama hawa nilikuwa natembea na bakora uwanjani”-Edo Kumwembe

on

Jumanne ya October 16 2018 ni siku ambayo ulichezwa mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu kucheza michuano ya mataifa ya Afrika 2019 nchini Cameroon, hivyo Taifa Stars ilikuwa ni zamu ya kurudiana na Cape Verde uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Katika game hiyo Taifa Stars walilipa kisasi kwa kuifunga Cape Verde kwa magoli 2-0, magoli yakifungwa na Simon Msuva na Mbwana Samatta, ukiachana na ushindi huo kivutio alikuwa Feisal Salum ‘Fei Toto’ alipoingia dakika za mwishoni akitokea benchi.

Pamoja na kuwa nyota huyo hana uzoefu na mechi nyingi za kimataifa lakini alionekana kujiamini zaidi na kuuchezea mpira, mchambuzi wa masuala ya soka Tanzania Edo Kumwembe ameandika maneno haya ya kumsifia mchezaji huyo.

“Mtoto Mjinga mjinga sana huyu Fei Toto…watoto kama hawa zamani nilikuwa natembea na bakora tu uwanjani….”- Edo Kumwembe

 

View this post on Instagram

 

Mtoto Mjinga mjinga sana huyu Fei Toto…watoto kama hawa zamani nilikuwa natembea na bakora tu uwanjani….

A post shared by Edo Kumwembe (@edokumwembe) on

Samatta alivyofutwa miguu baada ya game

Soma na hizi

Tupia Comments