Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Breaking News

BREAKING: David Kafulila amejivua Uanachama wa Chadema

on

Habari zilizotufikia muda huu zinamuhusu David Kafulila, Mwanasiasa maarufu wa Tanzania ambae pia ni Mbunge wa zamani wa Kigoma Kusini.

Kafulila amejiondoa CHADEMA na baada ya maamuzi hayo ameeleza sababu kwamba kwa sasa vyama vya upinzani vinaonekana kupigwa ganzi na kupooza katika juhudi zake za kupambana na ufisadi na ghafla ufisadi sio agenda kuu tena ya vyama vya upinzani tena.

“Kwa kuwa sina imani tena na upinzani kama jukwaa salama la kupambana na ufisadi, nimeamua kwa hiari na utashi wangu kujivua uanachama wa CHADEMA kuanzia tarehe ya taarifa hii, nitatangaza kwa siku za hivi karibuni jukwaa jipya la harakati zangu dhidi ya ufisadi”

ULIPITWA? KAULI YA KWANZA YA ALBERT MSANDO NA PATROBAS BAADA YA KUJIUNGA NA CCM, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUWATAZAMA

BREAKING: Na hii ndio Kauli ya CHADEMA kuhusu Wanachama wake waliomia CCM

Soma na hizi

Tupia Comments