Habari za Mastaa

Rappa French Montana hatimaye apata Uraia wa Marekani

on

Rapper Maarufu kutokea Marekani French Montana ame-share good news na mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa instagram baada ya kupata rasmi uraia wa Marekani na hii ni baada ya kuishi nchini humo kwa muda mrefu na kuomba uraia kwa miaka 20.

French Montana ambaye ni mzaliwa wa Morocco alipata uraia huo na kula kiapo June 14,2018 mjini New Jersey nchini Marekani ambapo unaambiwa utaratibu wa kupata uraia huo ulianza February mwaka 2017.

Rapper huyo alizaliwa na kulelewa nchini Morroco na kuzamia nchini Marekani akiwa na umri wa miaka 13 na kusema kuwa alikuwa hafahamu lugha ya Kingereza lakini alijituma na kuhahakisha anafahamu vizuri lugha hiyo na kwa mafanikio aliyonayo ilikuwa ni kama ndoto kwake.

“AMERICAN DREAM, nchi ambayo ndoto zangu zimetimia, nilitokea Morocco nikiwa na umri wa miaka 13 sikujua hata Kiingereza bali tulikuwa na matumaini na mioyo yenye utajiri . Ilinichukua miaka 20 kufanya hii siku itokee nilijitoa kwa vitu vingi na hata wakati mwingine nilitakiwa kurudisha nyumbani”

“Lakini Mungu alikuwa na amlengo makubwa kuanzia sasa niite AMERICAN MONTANA”

Hamisa kazungumzia Nyumba anazomiliki, vipi thamani yake..?

Soma na hizi

Tupia Comments