Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Ujauzito wa Blac Chyna washangaza mashabiki

on

Miezi kadhaa iliyopita tetesi zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na mwanadada Blac Chyna kuwa mjamzito na mpenzi wake wa sasa YBN Almighty Jay lakini kwa sasa picha zinazosambaa zinathibitisha ukweli kuhusu tetesi hizo.

Blac Chyna alianza mahusiano mapya ya kimapenzi na YBN Almighty Jay mwanzoni wa February 2018 baada ya kuachana na Robert Kardashian October 2017 na taarifa zilizopo ni kuwa mimba hiyo ni ya mpenzi wake YBN Almighty Jay mwenye umri wa miaka 18.

Blac Chyna mwenye umri wa miaka 30 amefanikiwa kuwa na watoto wawili ambaye wa kwanza ni King aliyebahatika kuzaa na Rappa Tyga na wa pili ni Dream aliyezaa na Robert Kardashian na huyu atakuwa ni mtoto wake wa tatu.

Kutokana na Blac Chyna kuwa mjamzito na mtoto wa tatu mashabiki wameshangazwa na yeye kufikia maamuzi hayo ya kubeba mimba ya kijana mwenye umri mdogo na wengi kudai kuwa ni sawa na mtoto wake wa kumzaa.

Blac Chyna na mpenzi wake wa sasa YBN Almighty Jay

Blac Chyna na watoto wake King na Dream

Nini amfungukia Nay wa Mitego

Soma na hizi

Tupia Comments