PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Habari za Mastaa

Steve Nyerere amuita Muna mara tano, amtaka aache utoto

on

Baada ya July 5,2018 kupitia instagram account ya Muna Love ambaye ni mama mzazi wa Marehemu Patrick aliamua kuweka wazi suala la baba mzazi wa Patrick na kusema kuwa ni Casto Dickson na hivyo kuwataka watu waache maneno ili apumzishe mwanae kwanza.

Hii ni baada ya taarifa kuenea kuhusiana na mvutano uliokuwepo kuhusu baba mzazi wa Patrick kutokana na Peter Zacharia Komu kujitokeza na kudai ni baba mzazi wa Patrick hivyo Steve Nyerere ametumia ukurasa wake wa instagram kumuonya Muna aachane na mitandao ya jamii na amalizane kwanza na kipindi hiki cha masikitiko.

“Muna muna muna muna muna naomba unisikilize popote ulipo ,Huu muda si wakufukua makaburi , Wewe muna kwangu ni mama bora ulimpenda mwanao ulisimama na mwanao mpaka kipindi cha mwisho MUNGU akupe nguvu muna.”

“Muna embu kaaa tena chini jifikilie ulitumia nguvu akili na maarifa yako yote na WATANZANIA wakatokea kukusapoti kwa namna moja ama nyingine kila mtu ameguswa na msiba wa mwanao .ndani ya mnchi na mnje ya mnchi,” Steve Nyerere

“Basi nakuomba Muna tumia busara sana weka utoto pembeni,Mweke shetani pembeni shilikiano na MUME wako wa NDOA kumpumzisha mtoto wenu,Matatizo yenu wekeni kando kipindi hiki kigumu Muna msiwape watu faida Muna” Steve Nyerere

“Naimani umeokoka basi kwenye hili kuwa na HOFU na MUNGU,sizani Muna kama aya tunayo yasoma mara mtoto wa huyu mara wa huyu,mara niliolewa nikiwa na mimba kama yanakujenga .bali nazani yanabomoa heshima yako.Dada nakuomba Fumba macho hili lipite nazani ata Patrick uko alipo analia kuona mfarakano huuuu. Msimtese mtoto uko alipo tumieni busara sana”

“Baada ya maziko ayo mambo yenu mtaendelea nayo kwa sasa ushauri wangu ungana na family muweze kumpa heshima mtoto wenu inayo mmstahili. Washauri wa muna nawaomba unganeni na family ya peter kumpa heshima mtoto wenu inayo mmstahili sisi wangine tupo pande zote ila atupendezwi na haya tunayo yaona nilizani ni muda muafaka wote kukusanyika mwananyamala kwa piter kuhakikisha tunampumzisha kijana wetu asante”

Baada ya vuta nikuvute, Muna Love amemtaja baba wa mtoto

 

Soma na hizi

Tupia Comments