Tangaza Hapa Ad

AyoTV

VIDEO: Zitto Kabwe akielezea kuhusiana na hali ya siasa nchini

on

Leo October 6  2016 mbunge wa Kigoma mjini na kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amekaa kwenye Clouds 360 ya clouds TV na ametoa maoni yake kuhusu hali ya siasa nchini ilivyo ikilinganishwa na awamu zilizopita, Zitto amesema…….

>>>’hali imebadilika kwa sababu tuna serikali mpya na ina namna yake ya kufanya shughuli zake, kwa hiyo ni dhahiri kwamba namna ambavyo tulikuwa tunafanya siasa lazima ziwe tofauti na sasa hivi kwa sababu ajenda zimebadilika mfano ni ajenda ya kupambana na ufisadi ilikuwa ndio ajenda kuu ya vyama vya upinzani katika serikali ya awamu ya nne sasa hivi serikali yenyewe ndio inayopambana na ufisadi’

>>>’siasa za sasa hivi zinatakiwa ziwe za utekelezaji zaidi, kama wewe ni mbunge au ni diwani utaonekana ni mwanasiasa mahiri kulingana na namna gani umejibu changamoto za wananchi ambao unawaongoza kuliko ilivyokuwa miaka 10 iliyopita kwamba ni kwa namna gani unaibua uozo katika utendaji wa serikali kwa hiyo lazima kuwe na mabadiliko kidogo ya namna gani tunafanya siasa zetu’:-Zitto

ULIKOSA MAJIBU YA ZITTO KABWE KUHUSU KUFUKUZWA KWAKE BUNGENI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement