Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Mix

Wasanii hawa waitwa ofisini na Naibu Waziri Shonza

on

 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza, Leo January 7, 2018 amezungumza na waandishi wa habari na kutangaza kuwafungia baadhi ya wasanii na wengine kuwataka kufika ofisini kwake kutokana na makosa mbalimbali likiwemo suala la uvaaji wa nguo zisizo za staha.

Juliana Shonza amemtaka msanii Gigy Money kufika ofisini kwake ”Ninamtaka Msanii wa Bongo Fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money kufika ofisini kwangu mara moja sababu alitumiwa ujumbe lakini hakujibu,hivyo ajue kuwa hawezi kushindana na serikali,”

“Serikali inafuatilia kwa karibu wasanii wote wanaoweka picha za kukosa maadili kwenye mitandao na kuwachukulia hatua hivyo ninamtaka msanii Jane Rimoy maarufu kama Sanchi kufika ofisini kwangu haraka,” -Juliana Shonza

ALICHOKIONGEA MSANII ALIYEFUNGIWA NA SERIKALI MIEZI SITA

 

Soma na hizi

Tupia Comments